Kiungo wa Namungo fc John Mbisse!
ASFC

Kiungo Simba! Namungo wanastahili ubingwa FA.

Sambaza....

Kuelekea mchezo wa fainali utakaopigwa mkoani Rukwa-Sumbawanga kati ya Namungo fc na Simba kiungo wa Namungo amepiga mkwara kwa wapinzani wao Simba.

Kiungo mshambuliaji John Mbisse ambae amepitia Simba B kwasasa yuko Namungo amesema wanajua ubora wa Simba na aina ya wachezaji wao lakini wapo tayari kupambana nao na kubeba ubingwa wa FA.

John Mbise “Sisi kama timu tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunaibuka kuwa mabingwa wa FA japo tunatambua Simba ni timu kubwa na ni timu bora inawachezaji wazuri ila sisi malengo yetu ni kuwa mabingwa wapya wa michuano hii ya FA.”

John Mbisse.

Mchezaji huyo wa zamani wa Dodoma fc na Mshikamano amesema Namungo inastahili kuwa mabingwa wa FA kutokana na safari waliyoianza tangu mchezo wakwanza wa michuano hiyo.

“Ndio tunauhakika wa kuwa mabingwa wapya wa FA, tumedhamiria kubeba ubingwa huu mbele ya Simba tulishajiandaa tangu mapema.” Alimaliza kiungo huyo ambae kuna tetesi msimu ukimalizika huenda akatimikia nchini Estonia katika majaribio.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.