Uhamisho

Kiungo wa Yanga atimkia Ulaya!

Sambaza....

Kiungo wa zamani wa Klabu ya Simba Mghana James Kotei baada ya kutimka zake Africa Kusini katika klabu ya Kaiser Chiefs amepata dili jipya barani Ulaya.

James Kotei alikua akiitumikia Kaiser Chiefs ya Ligi Kuu nchini Afrika Kusini maarufu kama PSL iliyomsajili kama mchezaji huru akitokea klabu ya Simba sc baada ya kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Africa.

Baada ya kukosa nafasi katika klabu hiyo Klabu ya Yanga ilijaribu kumsajili katika dirisha dogo lakini jitihada zao ziligonga mwamba na sasa mchezaji huyo anaitumikia klabu ya FcSlavia Mozyr nchini Belarus.

James Kotei akiitumikia klabu yake mpya nchini Belarus.

Klabu ya Yanga ilivutiwa na Kotei na hivyo kufanya mazungumzo na Kaiser Chiefs ambao walikubali kumuachia kiungo huyo wa shoka lakini tatizo likaja kwa Kotei mwenyewe ambae hakukubali dili hilo la kujiunga na Yanga ambao ni mahasimu wakubwa na klabi yake ya zamani ya Simba sc.

Sasa James Kotei amejiunga na Slavia fc inayoshiriki Ligi Kuu nchini Belarus ikishika nafasi ya 8 ikiwa na alama 13 katika timu 16. Klabu hiyo ilianziashwa mwaka 1987 huku ikitumia uwanja wao wa nyumbani Stadion Yunost wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 5500.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.