Sambaza....

Klabu ya soka ya Liverpool ya England imefanikiwa kumsajili kiungo wa Brazil Fabinho aliekua Mónaco ya Ufaransa kwa ada ya €45 milioni kwa mkataba wa miaka mitano.

Mbrazil huyo aliechezea timu yake ya Taifa mara nne anaweza kucheza pia kama beki wa kulia amesema ” Nimesisimkwa kutokana na huu uhamisho. Hiki ni kitu mara kwa mara nilikua nahitaji, hii ni klabu kubwa. Miundombinu ya klabu ni ya kipekee.” Aliiambia tovuti ya klabu ya Liverpool baada ya kusaini mkataba.

Fabinho akisaini mkataba kuitumikia Liverpool kuanzia July 1 mwaka huu.

“Nitajitahidi kutengeneza história yangu ya soka hapa. Natumaini katika ngazi ya mtu binafsi, ninauwezo wa kushinda mataji katika klabu hii”.

Ikumbukwe pia kiungo huyu amekua katika rada za Manchester United chini ya Josse Mourinho  kwa takribani misimu miwili lakini wakashindwa kumsajili. Hivyo kitendo chá Liverpool kupata saini yake ni kama Manchester United wamezidiwa maarifa na mahasimu wao Liverpool.

Sambaza....