Uhamisho

Ni Okwa sio Okrah!

Sambaza....

Miongoni mwa vitu huwa mashabiki wa soka huwa wanapenda na kusubiri kwa hamu ni kuona sajili mpya katika klabu zao na kuwaona jinsi ambavyo watacheza na kuisadia timu.

Katika usajili wa Simba wa dirisha hili Simba mpaka sasa imesajili takribani wachezaji nane na miongoni mwao ni Nassoro Kapama, Victor Akpan, Habibu Kyombo, Mohamed Ouatara, Moses Phiri, Dejan halafu kuna Augustine Okra na Nelson Okwa.

Augustine Okrah

Kati ya sajili ambazo Wanasimba wengi walikua na shauku ya kumuona na pia wakiwatambia wenzao wa Yanga ni Augustine Okra kutoka Ghana.

Katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kwenye kilele cha Simba Day dhidi ya St George ya Ethiopia Okrah alianza katika kikosi cha kwanza akicheza kama namba kumi nyuma ya mshambuliaji (ambae alikua ni Kyombo).

Ile shauku na ya Wanasimba kumuona fundi wao Okrah haikutimizwa haswa kutokana na kiungo huyo kuonyesha kiwango cha kawaida katika mchezo ule sivyo ambavyo mashabiki wengi wa Simba walitarajia.

Nelson Okwa (mbele) akishangilia bao pamoja na Victor Akpan.

Okrah hakua na wakati mzuri sana katika kutengeneza nafasi za mabao, kupiga mipira iliyokufa wala kufunga yeye mwenyewe. Lakini kinyume chake aliwafurahisha na kuondoka na kijiji ni Nelson Okwa.

Okwa aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Kibu Denis, si tu alifunga goli lakini pia aliwakosha Wanasimba waliojitokeza uwanjani kwa kandanda safi alilolioyesha katika Dimba la Benjamin Mkapa.

Okwa ameonyesha ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa katika kupiga pasi, kupenya katika ngome ya wapinzani akiwa na kasi pamoja na ufundi wa hali ya juu katika miguu yake.

Kikosi cha Simba kwa msimu 2022/2023

Kinyume chake mashabiki wa Simba walijiandaa kupata burudani kutoka kwa Okrah lakini aliyeteka shoo nzima ya Simba Day na kuandika jina lake katika mioyo ya mashabiki wa Simba ni Nelson Okwa kutoka Nigeria.

Kazi sasa imebaki kwa kocha wa Simba Maki katika kupanga wachezaji wake haswa katika eneo la kiungo wa ushambuliaji la Simba ambalo lina utiriri wa wachezaji. Katika eneo hilo kuna mafundi kama Okrah, Okwa, Chama, Banda, Sakho, Kibu, Mwinuke na Phiri.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.