Uhamisho

Pesa ya KICHUYA, Inauwezo wa kununua kina KICHUYA 6 wengine.

Sambaza....

Shiza Ramadhani Kichuya ameondoka na klabu yake ya Simba sc kwenda Misri lakini hatorudi nao yeye atabaki nchini humo.

Baada ya jana kuwepo na taarifa ya Simba Sc kumuuza Shiza Kichuya katika klabu ya Pharco inayoshiriki ligi daraja la kwanza Misri.

Tovuti yako ya Kandanda. Co.tz uliamua kuwatafuta viongozi wa Simba kudhibitisha habari hii, tulifanikiwa kumpata CEO wa Simba.

Alithibitisha habari hizi kuwa ni kweli  Shiza Kichuya ameuzwa kwenye klabu hiyo inayoshiriki ligi daraja la kwanza Misiri.

Cletus Magori  “Prof Madundo Mtambo, wakala wake na Simba SC wanajua vizuri kuliko sisi! Wana taarifa nyingi kuliko sisi!”

“Kichuya ameuzwa Pharco lakini anatolewa kwa mkopo Enppi, Matajiri wa Petrol waliopo Premier League! Mshahara wake hata kama angekuwa mwanao ungemruhusu aende tu!”

Magori pia aliongea “Umri wa kucheza mpira sio mrefu hivyo! Mtambue tunaofanya maamuzi tuna taarifa zaidi ya hizi mnazozifamu kwa sababu taarifa zingine ni za kimkataba!

Na huu ni Mkataba mrefu wa miaka minne! Nimekumegea kidogo tu! Na pia Klabu tutakachovuna si haba tunaweza nunua Kichuya hata 6!”. Kwa maana hiyo Shiza Kichuya hatoonekana tena na klabu Simba kwa sasa baada ya kupata mwajiri wake mpya.”


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.