Uhamisho

Pogba atacheza na Fernandes!

Sambaza....

Mlinzia wa zamani wa klabu ya Manchester United Jap Stam amesema angependelea kumuona Paul Pogba akibaki Old Trafod kutokana na ubora mkubwa alionao Mfaransa huyo.

Jap Stam mlinzi wa Uholanzi na mchezaji wa zamani wa AC Milan hakusita kuonyesha imani yake kwa Pogba na kusema ni wakati sasa wa yeye kuonyesha ubora wake licha ya kubakisha mwaka mmoja katika mkataba wake.

Jap Stam “Ningependa kuona Paul anabaki kwa sababu nadhani ni mchezaji bora, watu wanatarajia mengi kutoka kwake na kuna upinzani mwingi kwake. Wakati mwingine unaweza kusema hiyo ni sawa lakini nyakati zingine ukosoaji anaopata sio sawa.

Paul Pogba wa Manchester United akipambana Geoffrey Kondogbia wa Valencia Valencia.

“Sijui nini kitatokea, kwa kweli. Anahitaji kupata usawa kwanza lakini ningefurahi ikiwa angekaa na kucheza msimu mwingine. Pogba ni mchezaji ambaye ni mbunifu, anayetaka kucheza kidogo kwa njia yake, na wakati mwingine unahitaji kumpa uhuru kidogo”

Stam pia hakusita kutamani kuona muunganiko wa Pogba, Mac Tominay na Bruno katika eneo la kati la United.

Bruno Fernandes

Jap Stam “Ukiangalia Fernandes, Pogba na McTominay, nadhani wale watatu kwa pamoja uwanjani wanaweza kupendeza sana. Fernandes angeweza kucheza saa  namba 10 na Pogba anaweza kucheza kama mmoja wa wachezaji wawili waliokaa kwenye uwanja wa kati.

Ana uwezo wa kwenda mbele, pia ili uweze kucheza na wachezaji wawili wa kushambulia wa uwanja wa kati ikiwa mambo yataenda vizuri, lakini sivyo anaweza kushuka karibu na McTominay na wanaweza kucheza na namba10 tu. ”

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.