Uhamisho

Ramadhani Kessy atua Mtibwa Sugar

Sambaza....

Aliyewahi kuwa beki wa Nkana FC msimu uliopita Ramadhani Kessy amejiunga na klabu ya Mtibwa Sugar ya mjini Morogoro. Ramadhani Kessy ambaye amemaliza mkataba wake na klabu ya Nkana FC ametua kwenye klabu ya Mtibwa Sugar akiwa mchezaji huru.

Ramadhani Kessy anaenda Mtibwa Sugar kuziba nafasi ya Kibwana Shomari ambaye kasajiliwa na Yanga. Awali ilisemekana Ramadhani Kessy angesajiliwa na Yanga.

Mwisho wa siku Yanga ikamsajili Kibwana Shomari na kumuacha Ramadhani Kessy ambaye alionekana kwenye mitaa ya klabu hiyo kongwe nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Mtibwa Sugar ni nyumbani kwa Ramadhani Kessy kwa sababu ndiyo sehemu ambayo alitokea kabla ya kwenda klabu ya Simba na baadaye kwenda Yanga ambapo baada ya hapo alitimkia Nkana FC ya Zambia.

Sambaza....