Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam imekanusha kutoa taarifa ya hali ya afya ya beki Erasto Nyoni na kusema kuwa taarifa ambazo zimeendelea kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii ni upotoshaji.

Kauli hiyo imekuja baada ya vyombo mbalimbali vya habari asubuhi ya leo kuandika kuwa Nyoni ambaye aliumia goti kwenye mchezo wa jana wa Mapinduzi Cup dhidi ya KMKM kuwa atakuwa nje kwa muda wa majuma matatu.

Simba kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter imesema kuwa bado taarifa kamili haijatolewa na kwamba pengine baada ya vipimo vya madaktari watatoa taarifa hiyo Jumanne kupitia kwa mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Haji Sandei Manara

“Kuna taarifa za upotoshwaji zinazoendelea kusambazwa mitandaoni juu ya majeraha aliyoyapata beki wetu Erasto Nyoni kwenye mchezo wa dhidi ya KMKM uliochezwa jana, Nyoni anaendelea na vipimo leo hapa Dar es Salaam na taarifa zaidi itatolewa kesho na Msemaji wa Klabu” imesema taarifa hiyo.

Sambaza....