Uhamisho

Tuna kikosi cha bilioni mbili na nusu!

Sambaza....

Hassan Bumbuli msemaji wa klabu ya Yanga ametamba na kutaja gharama za kikosi cha sasa cha Yanga na kuwaita Wananchi kwenda kukitazama katima kilele cha siku ya Wananchi kesho katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

Akiwa makao makuu ya klabu ya Yanga mitaa ya Twiga na Jangwani amesema wapinzani wajiandae kuwakababili huku akiulizia upande wa pili huko wakoje.

Feisal Salum

Hassa Bumbuli “Sisi kama Yanga tuko vizuri kikosi kimesajiliwa kwa gharama kubwa sana, nikwambie bwanamkubwa kwamba tuna kikosi cha zaidi ya Bil 2.5 msimu huu ambapo mnaenda kukutana nacho kesho. Sijui upande wenu na tuna kikosi ambacho kinajumuisha Mataifa nane ya Afrika, sijui upande wenu, mtatuambia lakini.

Hiki kikosi tunataraji kwamba tunakijenga msimu kwa ligi ya ndani lakini kiende kikachukue Ligi ya Mabingwa Afrika. Tuna Carlinhos, Tonombe Mukoko, Tuisila Kisinda Feisal Salum fundi wa mpira yupo pale, sijui nyinyi mnajiaandaje kutukabili.”

Carlinhos, Kisinda

Bumbuli pia amegusia mauzo ya tiketi na kusema zinakaribia kuisha hivyo wanaanza kufunga mauzo kwa baadhi ya madaraja uwanjani.

“Tayari tumeshafunga mauzo ya tiketi za VIP A na zile za Royal kwasababu zimejaa na tunaelekea kufunga mauzo ya tiketi za VIP B kwasababu nazo zinaelekea kujaa.” Hassan Bumbuli.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.