ASFC

Wababe nane wa Ligi hawa hapa.

Sambaza....

Michezo yote ya raundi ya nne ya kombe la FA maarufu kama Azamsports Federation Cup tayari imetamatika na wababe watakaokwenda robo fainali wamefahamika.

Shirikisho la soka nchini linatarajiwa kuendesha droo ya robo fainali pia kutaja uwanja utakaotumika katika michezo ya fainali na nusu fainali mapema mwezi huu.

 

Simba ndio waliokua wakwanza kufuzu robo fainali kwa kuiondoa African Sports kwa mabak manne kwa bila. Yanga nao waliwafuata kwa kuiondosha Tanzania Prisons kwa mabao manne kwa moja kabla ya Geita Gold nao kuifusha Green Worriers.

Ihefu na Singida na wamefuzu kwa ushindi wa bao moja bila mbele ya Pan Afrika na JKT Tanzania. Wakati Mtibwa wao waliwatoa KMC wakiwa nyumbani.

Mbeya City wamefanikiwa kuwatoa Kagera Sugar na kuwa timu pekee iliyopata ushindi ugenini katika hatua hii. Azam Fc imekamilisha timu nane za robo fainali kwa kuwafunga Mapinduzi  Fc kwa mabao mawili kwa sifuri.

Sambaza....