Uhamisho

Yanga wamkana Tuyisenge!

Sambaza....

Baada ya tetesi kuzagaa kuhusiana na usajili utakaofanywa na klabu ya Yanga katika dirisha kubwa lijalo la usajili kocha wa Yanga Mwinyi Zahera akanusha tetesi hizo.

Kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera akiongea leo amesema kuna gazeti moja la michezo linaongea habari za uongo kuhusu Yanga.
Mwinyi Zahera “Kuna gazeti moja linaongea habari za uongo, linaandika habari kuhusu wachezaji tunaotaka kuwasajili si za kweli.”

Zahera pia aliongeza “Wanaongea kuhusu wachezaji kutoka Zambabwe na wengine Kenya sijui, hapana Yanga hatuna mpango huo. Kitu tunaongea ndani ya Yanga hakiwezi kufika kwenye magazeti sio ukwelii Yanga haijsajili yoyote.”

Jacques Tuyisenge mshambuliaji wa Gor mahia

Klabu ya soka ya Yanga imekua katika mawindo ya kimyakimya ya wachezaji wanaowataka kuwasajili ilo kuepusha kupokwa tonge mdomoni na watani zao Simba kutokana na nguvu ya pesa walionayo chini ya Mo Dewji.

Baadhi ya nyota wanaowapigia hesabu ni mlinda mlango wa Bandari fc ya Kenya  na mshambuliaji wa Gor mahia Jacques Tuyisenge


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.