Uhamisho

Simba na Yanga Kumgombea kiungo wa Azam

Sambaza....

Kiungo wa Timu ya taifa ya Zanzibar aliepo kwa mkopo Singida utd akitokea Azam fc Mudathir Yahya mkataba wake umefikia tamati na matajiri wa jiji Azamfc ulioisha tangu mwezi November mwaka jana.

Afisa habari wa Azamfc Japhar Idd  amethibitisha kua mchezaji huyo amemaliza mkataba nao, hivyo yupo huru kusaini mkataba na timu yoyote ile.

”Mkataba  kati ya Azam na Mudathir Yahya umekwisha, kwa kifupi ni kwamba mchezaji huyo ni huru anaweza kwenda kucheza timu yoyote kwa ajili ya maendeleo yake ya soka” Japhari Idd.

Image result for mudathir yahya images

Kwa kauli hiyo basi vinaipa nafasi nafasi vilabu vya Simba Yanga na Singida utd alipo sasa kwa mkopo kutafuta saini yake kwa nguvu ili kuwatumikia msimu ujao wa ligi.

Yanga bado wanatafuta mbadala wa Kamusoko ambae umri umemtupa mkono na akiwa anaandamwa na majeruhi ya mara kwa mara, hivyo kiungo kufanya kumtolea macho Mudathiri kuziba pengo la kamusoko.

Pia Simba itataka kusuka kiungo chake upyaa baada ya Said Ndemla kumaliza mkataba wake pia na Mwinyi Kazimoto umri kumtupa mkono. Hivyo huenda vita ya usajili ikaanza mapema kwa Simba na Yanga kusaka saini ya kiungo fundi Mzanzibar.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x