Baada ya kufanikiwa kuwaondosha Burundi katika hatua ya awali sasa Tanzania inasubiri upangwaji wa makundi ili kuweza kuanza safari ya kufuzu kombe la Dunia nchini Qatar.
Licha mwalimu wa Kili Stars kufanya mabadiliko kadhaa ya kuwaingiza Eliuta Mpepo, Hassan Dilunga na Ditram Nchimbi lakini juhudi zao hazikuzaa matunda na hivyo kupelekea kupoteza alama zote tatu!
Kipa wa Zanzibar pia ameonyesha kiwango kizuri katika mchezo huo kwa kuokoa michomo hatari katika lango na kuifanya Zanzibar kuambulia walau alama moja.