Mbeya City vs Singida United
Ni Mechi ya KUJINASUA…
Timu zote zinapatikana katika ukanda wa hatari. Mbeya City tayari imeshacheza michezo 10 ikiwa na alama zake 8 katika nafasi ya 18 huku Singida United imeshacheza mechi 11 ikiwa na alama 4 pekee katika nafasi ya 20 yaani ya mwisho katika msimamo wa ligi.
Biashara United vs Mtibwa Sugar
Huenda ikawa mechi ya Muendelezo wa Ushindi kwa Kocha Zuberi Katwira, baada ya kupata ushindi wa goli 1-0 katika mechi iliyopita dhidi ya Mwadui FC katika dimba jipya la CCM Gairo.