Ligi Kuu

Jinsi Simba walivyoweka rekodi ngumu ya mabao Ligi Kuu

Sambaza....

Wekundu wa Msimbazi Simba wanaendelea na harakati zao katika kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC ambapo wana kazi kubwa yakumfukuza Yanga aliyekaa kileleni  kwa tofauti ya alama nane.

Katika Ligi hiyo ambayo Yanga anaongoza kwa alama, Simba wao wameamua kutengeneza utawala wao katika ufungaji wa mabao na kuwa timu iliyofunga mabao mengi mpaka sasa wakiwa na mabao 58.

 

Mpaka sasa katika Ligi Kuu ya NBC zimefungwa hatrick sita kutoka kwa wachezaji watano tofauti wakitoka katika timu tatu tofauti za Ligi. Katika hatrick zote hizo Simba ndio inaongoza kwa kutoa wachezaji wengi waliofunga hatrick.

Kwenye wafungaji sita wa hatrick mpaka sasa Ligi ikiwa inaendelea Simba imetoa wafungaji watatu huku Jean Baleke akiongeza baada ya kufunga mabao matatu katika mchezo dhidi ya Mtibwa. 

Fiston Mayele akishangilia bao lake dhidi ya Singida Big Stars.

Baleke anaungana na John Bocco mwenye hatrick mbili na Saidoo Ntibazonkiza. John Bocco alifunga hatrick katika michezo dhidi ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting wakati Saido yeye aliwafunga Tanzania Prisons.

Kwa upande mwingine hatrick nyingine mbili zimetoka klabu ya Yanga na Namungo Fc. Fiston Mayele aliifungia Yanga mabao matatu dhidi ya Singida Big Stars wakati Ibrahim Mukoko yeye aliifungia Namungo dhidi ya KMC.

Ibrahim Mukoko akikabidhiwa mpira na mwamuzi katika mchezo dhidi ya KMC baada ya kufunga mabao matatu “hatrick”

Katika hatrick zote tatu Jean Baleke anaweka rekodi ya kipekee yakufunga hatrick mkoani [Morogoro] kwani hatrick nyingine zote tano zimefungwa ndani ya Jiji la Dar es salaam katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na moja ikifungwa uwanja wa Uhuru katika mchezo wa KMC na Namungo.

Sambaza....