Serie A

Mancini alaani vitendo vya kibaguzi kwenye soka.

Kocha wa timu ya Taifa ya Italy Roberto Mancini amesema kitendo cha ubaguzi alichofanyiwa mshambuliaji kinda wa Juventus Moise Kean sio cha kuvumiliwa hata kidogo. Mancini amesema adhabu kali na nzito inatakiwa kutolewa kwa mashabiki wa Cagliari ili kuzia tukio kama hilo ambalo limetokea kwa mara ya tatu ndani ya...
Mataifa Afrika

Uganda waipandisha Tanzania viwango vya soka Ulimwenguni.

Ushindi wa Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Uganda kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kwenye fainali za Mataifa Afrika (AFCON) umeifaidisha si tu kufuzu bali hata kupanda kwenye nafasi za ubora wa soka Ulimwenguni. Viwango hivyo vinavyotolewa na shirikisho la Kandanda Ulimwenguni (FIFA)...
EPL

Ukame wa mabao kwa Salah, wamlazimisha Klopp kuzungumza!

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema haoni kabisa kama mshambuliaji wake raia wa Misri Mohamed Salah anasumbuliwa na tatizo la msongo wa mawazo kutokana na kushindwa kuzitingisha nyavu katika michezo nane iliyopita. Salah ambaye msimu uliopita alifunga mabao 44 katika mashindano yote, msimu huu umekuwa mgumu kwake akifunga mabao 20...
EPL

Hawa ndio nyota sita, wanaoondoka Manchester United.

Klabu ya soka ya Manchester United ipo mbioni kuwaachia nyota wake sita katika kipindi cha majira ya joto kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuisha mikataba, kupungua viwango vyao pamoja na sababu nyingine mbalimbali. Nia hiyo ni maalumu kwa ajili ya kumsaidia Kocha Ole Gunnar Solskajaer kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi...
EPL

Ole: United inahitaji alama 15 kuingia ‘Top Four’!

Meneja wa klabu ya soka ya Manchester United Ole Gunnar Solskajaer amesema ili waweze kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye ligi kuu England ni lazima washinde michezo mitano kati ya sita ambayo imebaki. Ole ameyasema hayo baada ya timu yake kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Wolverhampton Wanderers...
Serie A

Mchezo wasimama dakika tatu, Kean akiimbiwa nyimbo za kibaguzi.

Mchezaji kinda wa Juventus Moise Kean jana amekutana na wakati mgumu baada ya mashabiki kumtolea maneno ya kibaguzi wakati timu yake ikiwa uwanjani ikipambana na Cagriali kwenye muendelezo wa ligi kuu nchini Italia. Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 alionekana akiushika mkono wake baada ya kufunga bao la pili,...
Ligi Kuu

Ooohoo!!! Simba waifuata Mbao na hasira kibao.

Kikosi cha wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club kimeondoka leo asubuhi kikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Morogoro ambapo watacheza mchezo wa ligi dhidi ya Mbao FC kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Humo. Meneja wa timu hiyo Patrick Rweymamu amesema wachezaji wote waliosafiri leo asubuhi wapo katika hali nzuri...
EPL

Ole apewa rasmi usukani wa Manchester United.

Klabu ya soka ya Manchester United imemtangaza kocha Ole Gunnar Solskjaer ambaye alikuwa akikaimu nafasi ya umeneja toka kuondoka kwa Jose Mourihno kuwa meneja wa kudumu kwa mkataba wa miaka mitatu. Kocha huyo ambaye alikuwa akiifundisha Molde ya nchini Norway toka mwaka 2015 amechukua rasmi mikoba ya Jose Mourihno katika...
1 2 3 4 5 6 34
Page 4 of 34