Toka mwaka aliosajiliwa yaani 2013, Fellaini amekuwa si chaguo la mashabiki wa Manchester United licha ya makocha wote watatu David Moyes, Louis Van Gaal na Jose Mourihno wakimtumia katika mechi muhimu
Akiwa katika ligi kuu nchini Uchina aliiwezesha klabu ya Shanghai SIPG kutwaa ubingwa msimu uliopita akifunga mabao 27 na pia kutwaa kiatu cha mfungaji bora.
Katika msimamo wa kundi D Simba inashika nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo miwili, wakishinda mchezo mmoja dhidi ya Jeunesse Sportive de la Saoura kwa mabao 3-0 jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda kupokea kichapo kikali cha mabao 5-0 kutoka kwa AS Vita ya nchini DR Congo
Mabao ya Simba katika mchezo huo yamepatikana kupitia kwa Emmanuel Okwi na Cletous Chama, na sasa Simba wamekata tiketi ya kucheza nusu fainali na Bandari FC waliowatoa Singida United.