Blog

Nantes watozwa faini kwa kuomboleza kupotea kwa Emiliano Sala.

Klabu ya soka ya Nantes ya nchini Ufaransa imepigwa faini kwa kosa la kuwasha mioto wakati wakiombeleza kupotea kwa mshambuliaji wao Emilliano Sala mwezi uliopita. Shirikisho la sok nchini Ufaransa limeitoza klabu hiyo faini ya shilingi milioni 43.7 baada ya mashabiki wake kuwasha baruti na mioto katikati ya bango kubwa...
Serie A

Timu iliyobugizwa 20-0 yaondolewa kwenye ligi nchini Italia.

Unaikumbuka ile timu ambayo ilifungwa mabao 20-0 mwishoni mwa juma hili kule nchini Italia? Basi imeondolewa kwenye ligi. Timu hiyo kwa jina la Pro Piacenza imeondolewa kwenye ligi baada ya kubainika imechezesha wachezaji saba pekee kwenye mchezo huo ambao walifungwa na timu ya Cuneo katika ligi daraja la tatu nchini...
Blog

Henry akingiwa kifua na Babu Wenger.

“Thierry Henry ana sifa zote za kuwa kocha mzuri na mwenye mafanikio” ni kauli ya kocha Arsene Wenger aliyoitoa Jumapili alipoulizwa kama kutimuliwa kwa Henry katika klabu ya AS Monaco kunaweza kumuathiri na kuharibu maisha yake ya ukocha. Wenger mwenye umri wa miaka 69 amesisitiza kuwa Henry bado ni kocha...
EPL

Ole: Mpeni muda Sanchez.

Kocha wa muda wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema anaamini kiwango cha mshambuliaji wake Alexis Sanchez kitaimarika licha ya kutupiwa lawama na mashabiki wake kutokana na kucheza chini ya matarajio ya wengi. Sanchez ambaye ni raia wa Chile alisajiliwa na Manchester United katika dirisha dogo la usajili mwaka jana...
Ligi Kuu

MZFA Watoa ufafanuzi, kutokuwapo kwa Ambulance Kirumba.

Chama cha soka mkoa wa Mwanza (MZFA) kimetolea ufafanuzi kuhusiana na kutokuwapo kwa gari la wagonjwa (Ambulance) kwenye uwanja wa CCM Kirumba wakati Mbao FC wakicheza na Coastal Union ya Tanga kwenye michuano ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara. Katibu Msaidizi wa MZFA Khalid Bitebo amesema ni kweli gari la...
Blog

Wakina Solskjaer wamchefua Rais wa UEFA.

Rais wa Shirikisho la soka Barani Ulaya (UEFA) Aleksander Caferin amehuzunishwa na kitendo kilichofanywa na makocha wa timu kubwa barani humo cha kushindwa kuhudhuria mkutano wa kujadili matumizi ya Teknolojia ya Kumsaidia Mwamuzi (VAR). Caferin amesema kitendo walichokifanya Mameneja hao ni kama dharau kwa UEFA na mpira kwa ujumla kwani...
EPL

Polisi wathibitisha kifo cha Emiliano Sala.

Mwili ulioopolewa kutoka kwenye ndege umetambuliwa kuwa ni mshambuliaji wa Cardiff City Emiliano Sala, kama taarifa zilivyothibitishwa na kituo kikuu cha Polisi mjini Dorset. Mwili huo hapo awali ulitambuliwa kuwepo kwenye ndege siku ya Jumatano na juhudi za kuutoa zilizaa matunda jana Alhamis na baada ya hapo ukapelekekwa kwenye uchunguzi...
EPL

Mwili mmoja waopolewa, ajali ya ndege ya Emiliano Sala.

Mwili ulioonekana kwenye ndege iliyopata ajali siku chache zilizopita umeopolewa kutoka kwenye ndege iliyopata ajali iliyokuwa imembeba mchezaji mpya wa timu ya soka ya Cardiff City, Emiliano Sala na Rubani David Ibbotson. Meli ya The Geo Ocean III iliyokuwa ibeba mwili huo iliwasili katika Bandari ya Portland mjini Dorset leo...
Ligi Kuu

Yanga wachoshwa na danadana za Beno Kakolanya.

Uongozi wa klabu ya Yanga umekiri kupokea barua nyingine kutoka kwa golikipa namba moja wa timu hiyo Beno Kakolanya ya kutaka kuvunja mkataba wake licha ya kulipwa stahiki zake alizokua akiidai klabu hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo kariakoo jijini Dar es salaam, Kaimu...
Ligi Kuu

Simba kumuuza Shizya Kichuya nchini Misri.

Klabu ya soka ya Simba imethibitisha kupitia mtandao wake wa Twitter kuwa ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na klabu ya Pharco ya nchini Misri kuhusu uhamisho wa winga Shiza Kichuya kwenda kujiunga na timu hiyo. Simba imesema kwamba taarifa zaidi itatolewa baadae baada ya taratibu zote kukamilika, kwa kiungo huyo...
1 6 7 8 9 10 34
Page 8 of 34