Al Alhly ndiyo mabingwa wa kihistoria wa kombe hili la ligi ya mabingwa barani Afrika. Kombe hili huwa wanalichukulia kwa maanani sana. Siyo rahisi kwao wao kukubali kupoteza nyumbani tena dhidi ya Simba.
Shungu ni kocha msaidizi wa AS Club Vita pia alishawahi kuifundisha Yanga SC miaka ya 99 anasema kuwa, Simba ni timu nzuri lakini wanacheza mpira laini “Soft Football
kula viporo vyake vitatu, dhidi ya Mwadui, Azam na Lipuli na lolote linaweza likatokea, kwa jinsi ligi ilivyo ni sawa na familia ya Kambare, mtoto ndevu na baba ndevu, wote wababe.
Katika msimamo wa kundi D Simba inashika nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo miwili, wakishinda mchezo mmoja dhidi ya Jeunesse Sportive de la Saoura kwa mabao 3-0 jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda kupokea kichapo kikali cha mabao 5-0 kutoka kwa AS Vita ya nchini DR Congo