Wenger tazama muda umekuacha
Miaka 21 imepita, miaka yenye rangi mbili ndani ya maisha ya Arsene Wenger ndani ya kikosi cha Arsenal. Hapana shaka rangi nyeupe ilitanda katika ngozi ya mwili wake ndani ya miaka 10 ya kwanza. Miaka ambayo alifanikiwa kupata mafanikio makubwa katika soka la England. Mafanikio ambayo yalimpa heshima kubwa sana...