Na kipigo cha mwisho ni dhidi ya Azam Fc katika nusu fainali ambapo Simba walipoteza kwa mabao mawili kwa moja na hivyo kuondoshwa kwenye kombe hilo na kuifanya Simba kutoka tena patupu msimu huu bila kombe lolote.
Katika msimu huu pekee Azam na Simba wamekutana mara tatu, mara mbili katika Ligi ambapo Azam alishinda mchezo wa kwanza na sare katika mchezo wapili na huu wa FA ambao Simba imetolewa.
Kwa upande wa Geita wao bado wanakumbuka walivyofungwa nje ndani na Yanga msimu huu lakini pia walovyotolewa msimu uliopita katika michuano hii hii hatua ya robo fainali na Wananchi Yanga.