Mfumo huu hutegemea utimamu wa viungo watatu wa kati ili kuleta “fluidity na Flexibility” ya timu . Timu itakuwa na uwezo wa kumiliki mpira, kukaba na kuufikisha mpira eneo wanalotaka.
TP Mazembe chini ya kocha Pamhile Mihayo Kazembe, inashika nafasi ya 2 katika msimamo wa Linafoot ikiwa na alama 58 wakicheza michezo 23 nyuma ya vinara AS Club Vita wenye alama 65 katika nafasi ya kwanza wakicheza michezo 25.
Simba inaenda kukutana Tp Mazembe katika mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam huku ikiwa na kumbukumbu nzuri baada ya kuwafunga Wacongo wenzao AS Vita katika dimba hilohilo la Taifa.