Falsafa ya Simba ni Kushambulia kwa kulimiliki eneo la kati, na ikitokea Simba wakamilikiwa kati, ujue kutakuwa hakuna ujanja mwingine. Acha tuzitazame mechi hizi ili kuliona hili… JS SAOURA VS SIMBA. Katika mechi hii Simba walilala kwa goli 2-0, huku eneo la kiungo wakianza na James Kotei na Jonas Mkude...
Usajili wa Simba unaonekana kuwa ni wa kimikakati zaidi, hasa kwa kuzingatia ripoti ya mwalimu na madhaifu yaliyojitokeza katika kikosi kwa msimu ujao kuanzia kwenye ligi hadi klabu bingwa Afrika.
Katika Chuji mmoja ulikua unaweza kupata viungo watatu kwa maana ya kiungo wa ulinzi, kiungo mchezeshaji na kiungo mshambuliaji, jamaa soka alilijua na lenyewe likamjua.