KMC FC vs Ruvu Shooting

Kmc kabla ya Ligi kusimama wamepata ushindi katika michezo minne ya mwisho huku pia wakifanya vizuri katika michezo ya kirafiki. Ruvu shooting wataingia na kujiamini kutokana na kupata sare na Simba mchezo wao wa mwisho

JKT Tanzania SC vs Yanga SC

Yanga wanameanza vizuri baada ya kuifunga Mwadui huku wakiwa bila nyota wao Benard Morrison, JKT Tanzania ipo uwanja wake wa nyumbani huku wakiwa katikati mwa msimamo wa VPL.

Azam FC vs Mbao FC

Azam fc inawania nafasi mbili za juu huku mshindani wake mkubwa Yanga akitoka kupata matokeo mchezo wa jana. Mbao fc wapo mkiani kabisa mwa msimamo wakijaribu kujinasua.

Simba SC vs Ruvu Shooting

Simba inataka kujihakikishia ubingwa mapema huku Ruvu Shooting wakiwa hawana uhakika wakisalia katika Ligi Kuu Bara kutokana na kua katika hatihati ya kucheza Playoff au kushuka kabisa.

Coastal Union FC vs Namungo FC

Coastal Union ilikua timu ya kwanza kuifunga Namungo fc katika uwanja wake wa nyumbani msimu huu. Je Namungo watalipa kisasi, huku wakiwa wanatofautiana alama moja tu katika msimamo.

Stori zaidi