Tayari kikosi cha Simba kimeshaanza maandalizi ya kushiriki michuano hiyo huku wakiwa tayari wanajinasibu wameanza usajili mzito kuelelea mashindano hayo.
Tangazo la kujiondoa lilikuja kupitia video ya Mortada Mansour, rais wa klabu hiyo, ambaye alifukuzwa kazi na Wizara ya Vijana na Michezo, kwenye chaneli yake ya YouTube.
Awali kulikua na katazo la mashabiki katika viwanja vya soka nchini Misri kutokana na sababu za kiusalama na kupelekea michezo mingi nchini huo kuhudhuriwa kwa idadi maalum ya mashabiki.
Simba itampasa kuchanga vyema karata zake katika mchezo wa kwanza kama kweli wanataka kwenda nusu fainali kwani wataanzia nyumbani mchezo wa kwanza na kumalizia ugenini mchezo wa mwisho.
Mashabiki wametambua nguvu yao katika mchezo huu na wametambua kuwa hiki ndo kipindi timu yao inawahitaji zaidi Uwanjani.
Ndo maana wamenunua tiketi kwa wingi tena ndani ya muda mfupi.