Martin Kiyumbi

Mchambuzi
Mchambuzi wa mpira wa miguu, mwenye Shahada ya Ualimu. Martin amejiunga na timu ya kandanda toka mwaka 2017, moja kati ya wachambuzi wakongwe katika familia yetu.
Blog

Naisubiri 2050 niisimulie hadithi ya Lionel Messi

Koti langu litakuwa nadhifu, sitoruhusu hali ya uchafu wa aina yoyote katika mwili wangu. Nitaonekana mzee- kijana. Mzee anayejipenda haswaa!. Mzee ambaye muda mwingi nitakuwa natumia kuangalia mifugo ambayo nitakuwa nashirikiana na mke wangu kuitunza. Mke ambaye amejaa upendo, mwenye kunijali, kuniheshimu na kunipenda kama ambavyo aliwahi kuapa mbele ya...
EPL

Mambo kumi yanayoisibu Man Utd.

Manchester United imekuwa timu ya kawaida kwa sasa, haiogopeshi tena kama kipindi kile. Kipindi ambacho kila ukiona taya la Sir Alex Ferguson unaona ushindi ndani yake. Ndicho kipindi ambacho timu ilikuwa inapigana mpaka dakika za mwisho, haikuruhusu neno kupoteza mchezo liwepo katika akili yao. Kwao wao kushinda mechi ilikuwa utamaduni...
EPL

Upendo wa mashabiki wa United ni mwanga kwenye giza la Martial

Upendo alianza kuutengeneza alipofika katika uwanja wa Old Trafford akiwa kama kijana mwenye kipaji cha hali ya juu. Kipaji ambacho kilibeba matumaini ya watu wengi. Kila mtu alimtazama katika jicho lake. Kuna watu walimtazama kama kijana ambaye atakuja kuisumbua dunia kutokana na kipaji chake kikubwa, na wengine walifikia hatua ya...
Blog

‘Gloves’ za De Gea zilikuwa katika mikono ya Kakolanya

Dunia imeshawahi kuwa na makipa wengi ambao macho yenu yalifurahia kuwatazama. Makipa ambao wana sanaa kubwa sana wakiwa langoni. Kwa bahati mbaya hawa watu huwa hawathaminiwi kwa kiwango kikubwa kama wachezaji wa ndani. Lakini ukweli unabaki pale pale kuwa golikipa ni mtu muhimu sana ndani ya timu husika. Hispania wanamtambua...
Mabingwa UlayaMkeka

Wazee wa kubeti, tumewawekea mkeka wa leo!

Bayern Munich vs Ajax. BAYERN MUNICH KUSHINDA. Mechi tano Bayern kashinda 3, sare moja na kafungwa 1. Ajax kashinda 4 kafungwa 1. Bayern hawajawahi kupoteza dhidi ya Ajax kwenye uwanja wake wa nyumbani katika mechi nne zilizopita. Akifunga magoli 11 na kuruhusu 2. Kwenye mechi za kwenye makundi Bayern Munich...
Ligi Kuu

Kuporwa Unahodha kulimjenga Jonas Mkude.

Masikio yetu yanapenda vingi sana vya kufurahisha, na muda mwingi masikio yetu hupenda kutabasamu. Ni ngumu sana kuweka tabasamu kwenye sikio lako kwenye dunia hii ambayo ina watu wengi ambao hawana upendo kwako. Muda mwingi wanawaza kukuumiza hata siku ambayo wakikuona uko sehemu ambayo ni juu hutamani kukushusha chini ambapo...
Ligi Kuu

Ni aibu kwa kiongozi kuuficha ukweli kwenye mambo ya kishirikina!

Sikukuu ya Simba na Yanga jana ilimalizika. Ushindani ulianza nje ya uwanja kabla hatujahamia ndani ya uwanja. Sehemu pekee ambayo ukweli huwa haujifichi. Huwezi kuficha ukweli ndani ya uwanja kwa sababu ndiyo sehemu pekee ambayo nyeusi huonekana nyeusi na nyeupe huonekana nyeupe. Ndiyo sehemu ambayo mara nyingi huwa inatuhukumu sisi...
Ligi Kuu

Mambo matano niliyojifunza katika mchezo wa Simba na Yanga!

1: Tuna safari ndefu sana kuifikia pepo kama bado tunaamini giza lina nafasi kubwa katika mpira wetu. Ni ngumu kujenga timu yenye ushindani kimataifa kwa kuamini katika nguvu za giza kama ndiyo njia sahihi kwetu sisi kutupa ushindi. 2: Inawezekana Beno Kakolanya kaimbwa sana kuliko mchezaji yeyote katika mechi ya...
1 60 61 62 63 64 79
Page 62 of 79