Martin Kiyumbi

Mchambuzi
Mchambuzi wa mpira wa miguu, mwenye Shahada ya Ualimu. Martin amejiunga na timu ya kandanda toka mwaka 2017, moja kati ya wachambuzi wakongwe katika familia yetu.
Blog

Ujio wa Manji ulikuwa Sinema ya Yanga?

Asubuhi ya Agosti 17 ilikuwa ndiyo siku ambayo tulikuwa tunahesabu masaa kwenda uwanja wa Taifa kushuhudia mechi kati ya Yanga na USM Alger's. Na ndiyo siku ambayo wana Yanga wengi walipatwa na mshangao wenye maswali mengi, maswali ambayo mpaka sasa inawezekana hakuna mwenye majibu sahihi. Ni siku ambayo kurasa za...
Ligi Kuu

Anachokisubiri Djuma ni ufalme tuliomwahidi

Joseph Omong, jina ambalo lilikuwa na ukakasi mkubwa ndani ya masikio ya mashabiki wengi wa Simba. Hawakutaka kumsikia katika masikio yao, hata macho yao waliyatia upofu ili mradi wasimuone tu. Ilikuwa inakera kwao kumuona Joseph Omong katika benchi la ufundi. Kwao wao hawakukumbuka rekodi ambazo Joseph Omong aliwahi kuziweka huko...
La Liga

Koti la Ronaldo lilikuwa limemficha Benzema

Ndiyo usajili wa gharama msimu huu na ndiyo usajili ambao kila kona ulikuwa gumzo. Kila mtu alishangaa kwanini Cristiano Ronaldo anaenda Italy, nchi ambayo kwa miaka ya hivi karibuni ushindani umekuwa finyu. Juventus ameitawala ligi hii, hakuna ambaye ameweza kumzuia. Kila asubuhi pakikucha anawaza ashinde magoli mangapi. Hali ambayo imemfanya...
Blog

‘Press’ ya leo ilikuwa na Sura ya ‘Kamati ya Harusi’.

Hapana shaka siyo mara yako ya kwanza kuona hili neno kwenye makala zangu "kila kitu kwenye dunia hii ya sasa ni biashara". Ndicho kitu ambacho mimi nakiamini kwa sababu tuko kwenye dunia ya aina hii. Dunia ambayo watu wengi hufikiria kufanya chochote ili wapate faida. Faida ambayo huja baada ya uwekezaji...
Blog

Wachezaji watano wanaofaa kurithi Jezi ya Ronaldo

Hatunaye tena, yupo zake akiwa amekaa kwenye nyumba ya kibibi, kibibi kizee cha Turin. Miaka 9 aliitumia kujenga na kuweka alama ambazo zitakumbukwa na kila kizazi cha mpira wa miguu. Kitabu chake cha historia RealMadrid kilianza kuandikwa kwa dau ambalo lilimtoa Manchester United kuja RealMadrid. Dau ambalo lilimfanya kuwa mchezaji...
EPL

Mourinho, Kocha bora wa kujizuia aliyepoteza nguvu zake.

José Mário dos Santos Mourinho Félix ndiyo majina ambayo alipatiwa miaka 55 iliyopita. Ilikuwa ni ngumu kugundua mapema kuwa huyu atakuja kuwa kocha bora duniani. Kocha ambaye alikuja katika kipindi ambacho vijana wengi walikuwa hawapewi nafasi ya kuwa makocha wakuu katika timu zao. Mikono yake ilifanikiwa kufuta hiyo dhana, kila...
Ligi Kuu

Inawezekana Salum Chama hajui umuhimu wa waamuzi.

Ligi haina mdhamini mkuu, hiki ni kitu ambacho kinaumiza kichwa sana. Ligi yenye timu 20, timu ambazo zinatoka katika mikoa mbalimbali, mikoa ambayo miundombinu yake siyo rafiki kwa kiasi kikubwa. Miundombinu ambayo inafanya timu nyingi zipate gharama kubwa ya kuendesha timu. Makali ya gharama hizi yalitakiwa kupunguzwa kwa uwepo wa...
Ligi Kuu

Kuna wakati Manara anajing’ata ulimi wake.

Instagram ndiyo sehemu ambayo watu wengi maarufu hapa nchini kwetu hutumia kuonesha maisha yao binafsi na maisha ya biashara zao. Kwenye dunia hii ya sasa kila kitu ni biashara, na ili ufanikiwe kwenye kila kitu unachokifanya lazima ukifanye kwenye jicho la biashara. Ndiyo maana Diamond Platnumz aliondokana na dhana ya...
Blog

Tutumie hata kitabu cha Samatta kwa kina Ajib

Dibaji yake inavutia na haitofautiani sana na Dibaji za wachezaji wengi wa Tanzania. Hakuzaliwa katika mazingira yenye utajiri mkubwa, hata hakufanikiwa kuwa kwenye vituo vya kulelea na kukuza vipaji. Kwa kifupi ametokea kwenye mazingira halisi ya kitanzania. Mazingira ambayo vijana wengi hupitia. Mazingira ambayo yalimpa nafasi ya kucheza chandimu. Ndiyo...
1 59 60 61 62 63 74
Page 61 of 74
Tafadhali tumia viungo rasmi kusambaza habari zetu. Facebook, Twitter au Barua Pepe. Kama utataka kutumia habari zetu tuandikie kupitia habari@kandanda.co.tz