Tupilia mbali mbwembwe za mashabiki wa Arsenal sijui Lacanyavu,Auba,Xhaka boom, na wengine, hapo 2013 dunia ilizizima baada ya Mesut Ozil kutua rasmi kwa washika mtutu wa pale London.
Baada ya Nadri Haroub Ali “Cannavaro” kuagwa kwa heshima miaka michache ilyopita pale Jangwani alivyostafu basi angefuata Kelvin Patrick Yondani “Cotton”, ila mambo hayakuwa hivyo.
Akiwa ameshacheza mechi kadhaa za timu ya Taifa la Italia kuanzia kwa vijana hadi wakubwa, lakini kwa klabu mambo yalikua bado apeche alolo kwa mzaliwa huyo wa Torre Annunziata pale Italy
Mipango yote ya ile ‘sex football’ wanayotandaza Wanankurukumbi wale inaanzia kwake akipata mpira anaficha kwanza kisha anawastua Seseme, Awesu na Ally Kagawa anawambia ‘wazee mali hii hapa"