Tayari kikosi cha Simba kimeshaanza maandalizi ya kushiriki michuano hiyo huku wakiwa tayari wanajinasibu wameanza usajili mzito kuelelea mashindano hayo.
Tangu ilipochukua ubingwa mwaka 2018 bado haijawa tena tishio sana na kama Simba watakwenda Tunisia kucheza nao robo fainali itakua ni mara yao ya kwanza kwa miaka ya hivi karibuni
Simba itampasa kuchanga vyema karata zake katika mchezo wa kwanza kama kweli wanataka kwenda nusu fainali kwani wataanzia nyumbani mchezo wa kwanza na kumalizia ugenini mchezo wa mwisho.