Martin Kiyumbi

Mchambuzi
Mchambuzi wa mpira wa miguu, mwenye Shahada ya Ualimu. Martin amejiunga na timu ya kandanda toka mwaka 2017, moja kati ya wachambuzi wakongwe katika familia yetu.
Uhamisho

Yanga wamkosa Djuma

Aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa timu ya Simba, Masoud Irambona Djuma, amepata timu nchini Rwanda kwa mkataba ambao ni " mnono" kwa mujibu wa vyanzo vyetu. Irambona Masoud Djuma amesaini mwaka mmoja kuinoa timu ya AS Kigali. Ataanza kazi rasmi leo bila winga wa kushoto mrundi Emmanuel Ngama aliesajiliwa na...
Blog

Wenger rasmi kurudi January 2019.

Aliyewahi kuwa kocha wa Arsenal kwa muda wa miaka 22 mfululizo, Arsene Wenger Leo hii ameweka wazi kuwa atarudi rasmi mwezi wa kwanza mwaka 2019. Arsene Wenger mpaka sasa hajaweka wazi kuwa atarudi kama nani kwenye tasnia hii ya mpira. Kuna habari nyingi ambazo zinamhusisha kocha huyu aliyepata mafanikio makubwa...
Blog

Nilimsamehe Samatta baada ya Dakika 90

Kitambaa cha unahodha kilikuwa katika mkono wake wa kulia, kila jicho lilimtazama yeye kama kiongozi, kiongozi ambaye atakuwa mfano kwa wengine waliopo uwanjani. Kiongozi ambaye atakuwa wa kwanza kupigania nchi na wa mwisho kutakata tamaa. Kiongozi ambaye miguu yake haikutakiwa kuwa na neno "kukata tamaa". Miguu yake ilitakiwa ipigane sana...
Blog

Sura ya Nyoni inazeeka, Miguu inarudi utotoni

Rolling Stone ndiyo mahali sahihi ambayo unaweza kupataja kama chimbuko la Erasto Nyoni. Hapa ndipo yalikuwa machimbo sahihi yaliyotumika kuchimba hili dini. Dini ambalo limekuwa faida kwa muda mrefu katika taifa letu. Kuna wakati huwa tunalibeza sana, na kuna wakati mwingine dharau huvaa ndimi zetu na kufungua vinywa vyetu kwa...
Blog

Nyoni atasaidia vipi Taifa Stars?

Jana beki wa Simba Erasto Nyoni alijumuishwa rasmi katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars". Uteuzi ambao unaonekana kuwa na nguvu katika maeneo yafuatayo. 1: ENEO LA BEKI WA KATI. Timu ya taifa ya Tanzania " Taifa Stars" katika mchezo uliopita ilionesha nidhamu mbovu katika eneo la...
Blog

Kessy na Ulimwengu kuikosa Cape Verde

Beki wa kulia wa Timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars" anayecheza soka la kulipwa nchini Zambia, Hassan Kessy na mshambuliaji wa timu ya taifa Thomas Ulimwengu anayecheza soka la kulipwa nchini Sudan wataikosa mechi ya marudiano dhidi ya Cape Verde itakayochezwa kesho Jumanne. Wachezaji hao wote wawili wana kadi...
Blog

Erasto Nyoni aongezwa Taifa Stars

Kocha Emmanuel Amunike amemuongeza beki wa Kati wa klabu ya Simba, Erasto Nyoni, katika kikosi cha Taifa Stars. Hii ni kuongoza nguvu katika kikosi cha Stars kwaajili ya mechi ya marudio dhidi ya Cape Verde jumanne hii. Katika mechi hiyo Taifa Stars itamkosa pia Hassan Kessy aliye na kadi mbili...
Blog

Uganda “Dhaifu” ilituaminisha kuwa tushafika!.

Dimba la Nambole ni dimba gumu sana kati ya madimba yote yaliyopo Afrika Mashariki na Kati. Ni dimba pekee ambalo timu ya taifa ya Uganda haijawahi kuruhusu kufungwa tangu mwaka 1997. Ni sehemu ambayo Waganda wengi wanaiamini sana kwa sababu huwatia faraja kila wanapoenda kuishangilia timu ya taifa. Misri alikufa...
Blog

Natamani leo Amunike awaite Ajib na Kichuya!

Macho yangu yalikuwa makini sana tulipokuwa kwenye dimba la Nambole. Dimba ambalo ni gumu sana. Nilijaribu kuiweka presha pembeni na kuamua kuwatazama vizuri Taifa Stars. Na ikizingatia ilikuwa mechi ya kwanza ya kocha kutoka Nigeria Emmanuel Amunike, nilitamani kumuona anawezaje kucheza katika mechi za ugenini. Mechi ambazo hana mashabiki wengi,...
Blog

Samatta, kuna leo moja tu ya kujenga kiti chako cha enzi!

Kuna vingi vinavyoenda na kubaki katika maisha yetu kama kumbukumbu inayodumu. Kumbukumbu ambayo ni ngumu kuisahau kwa sababu ya ubaya au uzuri wa tukio husika. Mara nyingi watu wazuri hawadumu ila vitu vyao vizuri wanavyovifanya hudumu kizazi baada ya kizazi. Kizazi chetu kinamkumbuka Peter Tinno kwa sababu moja tu alifanikisha...
1 58 59 60 61 62 79
Page 60 of 79