Tabiri matokeo kwa kuandika katika sehemu ya maoni ndani ya tovuti yetu tu ya mechi hiii. Mtu wa kwanza kuwa sahihi kabla ya mchezo kuanza atajipatia tiketi ya VIP B mechi ya Simba SC vs AS V.Club na Jezi ya Klabu ya Simba.
Ugumu wa mechi ya Simba vs As Club Vita utachagizwa na matokeo ya mechi za awali yaani Simba dhidi ya JS Saoura na AS Vita dhidi ya Al ahly. Jumla AS Club Vita wanaweza kupata alama 1-3 katika michezo yake miwili iliyosalia na mwisho wa siku kuwa na jumla ya alama 5-7.
kwa dunia ni ya 91, na kwa Misri ni ya kwanza pia. AS Club Vita kwa Afrika ni ya 5, kwa kongo ni ya 2 na duniani ni ya 176. JS Saoura ni ya 53 kwa Afrika, ni ya 4 kwa Algeria na ni ya 644 kwa dunia. Wakati Simba ni ya 326 kwa Afrika, ya 1 kwa Tanzania na ni ya 1817 kwa dunia.
Katika msimamo wa kundi D Simba inashika nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo miwili, wakishinda mchezo mmoja dhidi ya Jeunesse Sportive de la Saoura kwa mabao 3-0 jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda kupokea kichapo kikali cha mabao 5-0 kutoka kwa AS Vita ya nchini DR Congo
Katika magoli yote 12 ya Simba katika michuano hii, magoli 7 yamefungwa na washambuliaji ikiwa ni asilimia 58.3, na magoli 5 yametiwa kimyani na viungo, hii ni sawa na asilimia 41.7.