Martin Kiyumbi

Mchambuzi
Mchambuzi wa mpira wa miguu, mwenye Shahada ya Ualimu. Martin amejiunga na timu ya kandanda toka mwaka 2017, moja kati ya wachambuzi wakongwe katika familia yetu.
Blog

Messi na Ronaldo siyo chochote kwa hawa!.

Inawezekana ndiyo wachezaji ambao wamegawana mashabiki katikati kwa kipindi cha muongo mmoja uliopita kama walivyogawa katikati tunzo ya Ballon D'or ndani ya miaka 10 iliyopita. Miguu yao imetufurahisha sana, ikatuliza sana kwa furaha na huzuni na kupelekea upande mmoja wa mashabiki kuwa na chuki na Messi na upande mwingine kuwa...
Ligi Kuu

Kuvaa koti zuri juu ya shati chakavu hakutoisaidia Yanga.

Hakuna kitendawili tena kwenye maisha ya Yanga, kwao wao maisha yao siyo fumbo tena kama tafasri halisi ya maisha ilivyo. Wanaishi kwenye maisha yaliyowazi, maisha ambayo yanawafanya wasiwepo katika dunia ya tambo na furaha. Wameshachagua dunia hii isiyopendwa na wengi, dunia ya huzuni na majonzi, dunia ya masimango na kubezwa...
Uhamisho

Ngassa alitakiwa aje Yanga kama kocha mchezaji.

Mrisho Khalfan Ngassa jina ambalo liliandikwa katika mioyo ya mashabiki wa Yanga, ni ngumu kulifuta katika mioyo yao kwa sababu mhuri wa moto ulitumika kuweka chapa ya jina la Mrisho Ngassa kwao. Chapa ambayo ilitokana na kiwango cha wakati huo cha Mrisho Khalfan Ngassa, kiwango ambacho ƙkilimpa heshima ambayo ilimfanya...
Blog

Zinedine Zidane ang’atuka Madrid

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane, ameachana na klabu hiyo siku tano baada ya kuipa taji la tatu mfululizo la klabu bingwa Ulaya. Zidane alitangaza uamuzi huo siku ya Alhamisi mbele ya rais wa klabu hiyo, Florentino Pérez. "Nimechukua huu umuzi wa kutokuendelea msimu ujao. Kwangu mimi na kwa kila...
Mabingwa Ulaya

Tatizo lilianza kwenye chozi la Salah.

Mwanzo mwa msimu ulianza na tabiri nyingi kuhusu maisha ya Zinedine Zidane pale Santiago Bernabeau. Wengi waliamini miguu yake haiwezi kudumu kukanyaga nyasi za Santiago Bernabeu. Tulimpa mwezi wa kuwepo Santiago Bernabeu, tukampa wiki mbili, Mwisho wa siku tukampa mechi tatu lakini akili ya Perez haikuwa kama tulivyokuwa tunawaza na...
Ligi Kuu

Aliye karibu na Kichuya amng’ate sikio ‘fastaaa’.

Misimu miwili imeshakamilika akiwa katika ardhi yenye udongo mwekundu, udongo ambao upo kwenye mbuga ya msimbazi, mbuga pekee yenye mnyama mmoja yani Simba. Mbuga hii ina malisho ambayo yana unafuu kuzidi mbuga zingine za mikoani, ndiyo maana wengi wa wachezaji hutamani sana kuishi kariakoo wakiamini ni sehemu yenye unafuu mkubwa...
Mabingwa Ulaya

Ni Real Madrid tena? Au Liverpool?

Ulevi wa timu hizi kwenye Ligi ya Mabingwa utatia ugumu wa mchezo? Hapana shaka kwa sababu zinakutana timu ambazo ulevi wao mkubwa ni michuano hii ya Ulaya, damu huchemka na wehu uingia akilini mwa kila mchezaji wa timu hizi linapokuja suala la Ligi ya mabingwa barani ulaya. Real Madrid wanatafuta...
Ligi Kuu

Nilichojifunza kwenye kipigo cha Simba dhidi ya Kagera Sugar.

Leo hii Simba ilikuwa inacheza mechi ambayo wangekabidhiwa kombe lao , furaha kubwa kwao ilikuwa ni kukabidhiwa kombe wakiwa hawajafungwa hata mechi moja kwenye ligi kuu lakini Juma Kaseja akaharibu matamanio yao. Kipi nimejifunza kwenye mechi hii? 1: Hapana shaka Watanzania tunapenda matukio ya muda mfupi na siyo matukio ya...
1 48 49 50 51 52 61
Page 50 of 61
Tafadhali tumia viungo rasmi kusambaza habari zetu. Facebook, Twitter au Barua Pepe. Kama utataka kutumia habari zetu tuandikie kupitia habari@kandanda.co.tz