epl

epl

Antonio: Mapumziko katika kalenda ya FIFA yamekuwa Baraka kwetu.

Winga wa West Ham United Michail Antonio amesema mapumziko ya kupisha mechi za Kimataifa zilizokuwepo kwenye kalenda ya FIFA yamekuja katika muda sahihi kwa timu ambazo zilikuwa zimeanza vibaya kwenye ligi kuu ya England ikiwemo West Ham. Wagonga nyundo hao wa jiji la London wameanza vibaya kwa kufungwa michezo yote...
epl

Keita awaomba uvumilivu mashabiki wa Liverpool.

Kiungo wa Liverpool Naby Keita amesema anahitaji muda ili kuthibitisha ubora wake na kufidia ada ya uhamisho ya Dollar Milioni 63 ambazo zililipwa kumsajili akitokea RB Leipzig ya Ujerumani. Keita ambaye ni raia wa Gini ameyasema hayo wakati akihojiwa na Jarida la Klabu ya Liverpool wakati wakijiandaa na mchezo wa...
epl

Mzimu wa msimu wa tatu uko kwenye nyayo za Mourinho

Jose Felix Mourinho, Mreno mwenye mafanikio makubwa sana katika ngazi ya ukocha. Mafanikio ambayo yalianza kama kitu cha kushangaza kwa sababu aliwashangaza wengi kupata mafanikio makubwa akiwa na klabu ya FC Porto. Timu ambayo ilikuwa haidhaniwi kama inaweza kutoa ushindani kwa timu kubwa kama Realmadrid, Bayern Munich, Barcelona , Manchester...
epl

Haueni, Lallana kurejea uwanjani baada ya Mwezi mmoja

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Adam Lallana huenda akarejea uwanjani kuendelea na mapambano ya soka baada ya mwezi mmoja, kutokana na jeraha la nyonga alilolipata na kumsababishia kuondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England kinachojiandaa na mchezo wa ligi ya mataifa ya Ulaya (UEFA Nations League) dhidi ya...
epl

Keita ni Ukamilisho wa torati ya Van Djik

Vitu vingi viliongelewa sana , na kitu kikubwa ambacho kilikuwa kinazunguka katika vinywa vya watu wengi na kauli ya Jurgen Klop. Kauli ambayo aliitoa kipindi ambacho Manchester United wamemnunua Paul Pogba. Hakutaka kuamini kama soko la mpira wa miguu limefikia hatua ya klabu kutoa pesa kubwa kwa ajili ya kununua...
epluhamisho

Olympiakos wamkana Yaya Toure

Uongozi wa klabu ya Olympiakos ya Uguriki umeshindwa kutoa tamko lolote, baada ya kuhusishwa na mpango wa kutaka kumrudisha kiungo kutoka Ivory Coast, Yaya Toure. Toure, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru, baada ya kuachwa na mabingwa wa soka nchini England Man City mwishoni mwa msimu uliopita, amekua katika harakati...
epl

Kipatacho: Sare na Alliance ni ya malengo.

Meneja wa timu ya soka ya African Lyon, Adam Kipatacho amesema sare ya mchezo wao dhidi ya Alliance kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara uliofanyika CCM Kirumba ilipatikana baada ya lengo la kulilinda bao walilolipata kipindi cha kwanza kushindikana. Kipatacho amesema sio kwamba walizidiwa katika mchezo hadi kuruhusu...
epl

Mourinho, Kocha bora wa kujizuia aliyepoteza nguvu zake.

José Mário dos Santos Mourinho Félix ndiyo majina ambayo alipatiwa miaka 55 iliyopita. Ilikuwa ni ngumu kugundua mapema kuwa huyu atakuja kuwa kocha bora duniani. Kocha ambaye alikuja katika kipindi ambacho vijana wengi walikuwa hawapewi nafasi ya kuwa makocha wakuu katika timu zao. Mikono yake ilifanikiwa kufuta hiyo dhana, kila...
epl

Tatizo linaanzia kwenye Kivuli cha Ferguson

Alama yake aliitumia kuiweka kwa miaka 27, umri wa mtu mzima. Akili, nguvu na muda wake mwingi aliuwekeza katika maisha ya Manchester United. Ndiyo maana alifanikiwa kuwa kocha mwenye mafanikio makubwa sana katika klabu ya Manchester United Alihakikisha kila sekunde inayopita katika maisha yake ilikuwa ni muhimu kuwapa furaha mashabiiki...
epl

Tatizo gari alilopanda Pogba, Dereva ni Raiola!

Pesa zilianza kumzoea mapema sana. Hakuweza kukaa bila na pesa yoyote mfukoni mwake tangu akiwa mtoto. Kwake yeye pesa kilikuwa kitu muhimu sana kuliko mwanamke. Vijana wengi wanapofikia umri wa kubalehe huwa machizi wa kutamani kuwa na wanawake wengi, lakini kwake ilikuwa tofauti kabisa. Alikuwa binadamu mwenye asili nyingine na...
1 2 3 7
Page 1 of 7
Tafadhali tumia viungo rasmi kusambaza habari zetu. Facebook, Twitter au Barua Pepe. Kama utataka kutumia habari zetu tuandikie kupitia habari@kandanda.co.tz