Mfumo huu hutegemea utimamu wa viungo watatu wa kati ili kuleta “fluidity na Flexibility” ya timu . Timu itakuwa na uwezo wa kumiliki mpira, kukaba na kuufikisha mpira eneo wanalotaka.
Idadi kubwa ya magoli ligi kuu Tanzania bara anayo yeye, yeye ndiye mfungaji bora wa muda wote, anagoli zaidi ya 100. Mchezaji aliyezifunga goli nyingi timu za Simba na Yanga rekodi pia anayo yeye. Ni mchezaji bora wa msimu uliopita. Na ni kepteni wa timu kubwa kama Simba. Bado unamchukulia poa tu?.